MWOKOZI UMEOKOA
1. Mwokozi umeokoa
Nimekuwa wako wewe
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana kondoo.
Utukufu, Aleluya!
Sifa kwa mwana
Kondoo!
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa yesu!
2. Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtugemea
Nilipata Baraka.
3. Diama Namwegemea,
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemchemi
Itokayo Mwokozi.
4. Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe;
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure.
5. Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima.
6. Nalikua kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo,
Yesu akanifungua.
7. Sifa, ameninunua!
Sifa, nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana huhifadhi!
Sifa zake milele.




